Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepokea zaidi ya shilingi milioni 498 ikiwa ni fedha kutoka kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) na hii ni kwa mara ya kwanza kwa mwaka huu tangu zoezi hili lilipositishwa kwa muda mapema Februari mwaka Jana.
Akizungumza wakati wa utolewaji wa fedha hizo kwa walengwa, mratibu wa TASAF kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sekunda Kasese amesema wamepokea fedha hizo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mpango wa kunusuru kaya maskini zaidi Tanzania.
Fedha hizo hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha ya kaya hizo hasa upande wa elimu, afya pamoja na lishe, ambapo walengwa wanapopata fedha hulenga katika kuinua na kuimarisha familia zilizoko katika mazingira magumu.
"Tumepokea shilingi milioni 498,216,295 kwa ajili ya malipo ya walengwa wa kaya maskini zaidi kwa mwezi Machi hadi Aprili 2019 zikijumuisha malipo ya walengwa 6,223 pamoja na waliofanya ajira za muda 4,884.
"Malipo haya yalisimama kwa muda lakini hivi sasa yameanza tena, ndio maana tumeanzia malipo ya mwezi Machi mwaka jana ili kila mlengwa apate stahiki yake," alisema Kasese.
Zoezi hili la malipo ya TASAF kwa ajili ya walengwa wa kaya maskini linajumuisha jumla ya mitaa 73 iliyopo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma huku ikilenga kuboresha huduma ya afya, elimu pamoja na upande wa lishe kwa wanufaika wake.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.