TIMU ya Dodoma Jiji FC inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kuongoza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa saa kadhaa baada ya kuifunga Mtibwa Sugar ya Morogoro bao 1-0 na kufikisha alama 10 ambazo hakuna timu ilikua imezifikia kwa wakati huo mpaka baada ya Yanga kushinda mechi yake dhidi ya Azam na kurudi kwenye uongozi wa Ligi na Walima Zabibu kwenda kwenye nafasi ya pili.
Katika mchezo huo ambao ulikua na mvuto wa aina yake Dodoma Jiji ilipata goli kupitia kwa Seif Karihe aliyepokea pasi safi kutoka kwa Aboubakar Ngalema dakika ya 60 ya mchezo na kufunga goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata amewapongeza wachezaji wake Kwa kupambana kwani haukua mchezo rahisi lakini walitakiwa kushinda ili kujihakikishia nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Aidha Makata ameongeza kuwa hawaangalii hali ya timu wanayokutana nayo, iwe vizuri au vibaya wanachoangalia wao ni malengo waliyojiwekea kutimia na si vinginevyo.
"Uzuri wa kikosi changu unatokaana na uwepo wa wachezaji wanaojituma na kujua nini wanafanya, hatuna mchezaji mkubwa wala mtoto kwenye timu yetu wote ni sawa" alisema Makata.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.