MSAFARA wa Kikosi cha Dodoma Jiji FC chenye wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kimewasili salama Mkoani Rukwa kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo namba 225 wa ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa katika dimba la Nelson Mandela hapo kesho Jumamosi tarehe 10/04/2021 saa 8:00 mchana.
Akizungumza baada ya kuwasili Mkoani hapo Afisa Habari wa timu hiyo Moses Mpunga amesema kuwa Tanzania Prisons ni timu nzuri na ngumu ila uzuri na ugumu huo ndio utakaowafanya wao kuwa wazuri zaidi mbele Wajelajela hao na kuwatoa hofu mashabiki na wapenzi wa Dodoma Jiji FC kuwa wanakwenda kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao.
Mpunga ameongeza kuwa wataingia kwenye mchezo huo kwa tahadhali kubwa wakijua kuwa wapinzani wao wanauzoefu katika ligi hiyo hivyo umakini na nidhamu ya mchezo vitahitajika sana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo.
“Hatuko kwenye ligi Kuu kusindikiza au kuangalia wengine wakishinda hapana! Tupo hapa kupambana na kushinda tuna sababu nyingi za kutufanya tushinde hivyo watanzania watarajie mazuri kutoka kwetu kwani hii ni timu ya watanzania wote ukizingatia tunatoka Makao Makuu ya Nchi yao hivyo wana kila sababu ya kujivunia uwepo wetu kwenye ligi hii na tuna ahidi kuwapa raha” alimalizia Mpunga.
Aidha Dodoma Jiji inakutana na Prisons kwa mara ya pili katika msimu wa ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021 ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Dodoma kupoteza kwa kufungwa goli moja katika uwanja wa Samora Mkoani Iringa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.