AFISA na Mratibu TEHAMA kutoka TAMISEMI,Mwl. Mratibu Abed, amewataka walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wanaopata mafunzo ya TEHAMA kufanya kwa vitendo na kwa waledi ili waweze kwenda kusaidia wanafunzi mashuleni.
Hayo ameyasema leo oktoba 25, 2021 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa mafunzo ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa lengo la kufikisha elimu kwa walimu wengine kwa Sule za Sekondari na Msingi nchini.
Mwl Abed amewataka walimu kufanya mafunzo kwa umakini wa hali ya juu kwa vitendo ili waweze kufikisha elimu sahihi kwa wanafunzi ambao wataenda kuwafundisha na kuwa watatoka na kitu.
Aidha amewataka kuwa wavumiliu kwa changamoto zitakazojitokea kwa kipindi chote cha mafunzo pia kwa wale wasio na vifaa vya Tehama watasaidiwa kuweza kupata.
“Mafunzo haya ninyeti inawabidi kufanya mafunzo hayo kwa umakini wa hali ya juu kwa vitendo ili muweze kuelewa na kuwafkishia wanafunzi na walimu ambao mmewawakilisha”amesema Mwl Abed
“lakini pia kwa vikwanzo au changamoto yoyote mtakazo kutana nazo itawabidi kuwa wavumilivu lakni pia kwa wale ambao bado hawajapata vifaa vya Tehama tutawasaidia kuweza kupata,”amesema
Kwa upande wa walimu kutoka shule ya sekondari ya Wasichana Tabora,Daudi Njele , amesema wanatumani wanatweza kufanya vizuri mafunzo haya nawataweza kufanya kwa vitendo na umakini ili kufikisha elimu dhabiti kwa wanafunzi na walimu walio wawakilisha.
Aidha ameishukuru UCSAF kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wiki nzima maana inaenda kuwasaidia wao pamoja na wanafunzi kutokana na mfumo wa Dunia ya sayansi na teknolojia inavyohitaji
”Tunaishukuru UCSAF kwa kuanda mafunzo haya maana yataenda kutusaidi sisi pamoja na wanafunzi kutokana na mfumo wa Dunia ya sanyansi na teknolohia inavyohitaji,”amesema
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.