NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema Serikali inatambua umhimu wa motisha kwa Walimu hasa wale wanaofanya kazi vijijini kwa kuboresha mazingira yao ya kazi ili waweze kufanyakazi kwa hamasa.
Mhe. Katimba amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Nora Waziri Mzeru aliyetaka kujua Je,Serikali ina mkakati gani wa kuboresha Mazingira ya Kazi pamoja na motisha kwa Walimu hususani wale wanaofanyakazi Vijijini.
“Serikali inatambua umhimu wa motisha na kuboresha Mazingira ya Kazi kwa Walimu hasa wale wanaofanyakazi vijijini ili waweze kufanyakazi kwa hamasa, mkakati wa serikali katika eneo hili ni kujenga nyumba za kuishi katika maeneo yao ya kazi na kuendelea kuhakikisha kwamba walimu wanalipwa stahiki zao kwa wakati” Mhe. Katimba.
Aidha Mhe. Katimba amesema serikali itaendelea kutenga Fedha kila mwaka wa Fedha ili kuendendelea kujenga Bwalo na miundombinu mengine katika shule zisizokuwa na Bwalo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mhe. Dkt. Florence George Samizi aliyehoji Je, ni lini Serikali itajenga miundombinu ya shule ya Sekondari Mkugwa ikiwemo mabweni, Bwalo na Madarasa?
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.