WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amewataka walimu kote nchini Kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye Waraka namba 24 wa mwaka 2002 ambao umeeleza wazi ni nani mwenye Mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko na viboko Vingapi vinaruhusiwa na kwa utaratibu upi vinatolewa kwa wanafunzi.
Waziri Kairuki ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri kwenye kikao kazi cha uboreshaji wa Usimamizi wa Elimu Msingi na Sekondari Jiji la Dar es Salaam.
"Suala zima la adhabu ya Viboko mashuleni linaongozwa na Waraka wa Elimu namba 24 wa mwaka 2002 na umeeleza bayana kabisa"
Waziri Kairuki ameendelea kufafanua kuwa Waraka huo na Kanuni za Elimu za mwaka 2002 lazima zifuatwe katika utolewaji wa adhabu ya viboko mashuleni.
"Kwa Mujibu wa mwongozo huo umeelekeza adhabu hiyo ya viboko inaweza kutolewa pale ambapo umetokea utovu wa nidhamu uliokithiri au makosa ya Jinai yaliyotendeka ndani au nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia heshima shule" amesisitiza Kairuki.
Pia Waziri ameendelea kuelekeza kuwa "kwa mujibu wa Waraka huo adhabu hiyo inavyotolewa lazima izingatie vigezo ikiwemo ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na haipaswi kuzidi viboko vinne kwa wakati mmoja"
‘Waraka huo umeeleza jinsi adhabu hiyo inapaswa kutolewa kwa mtoto Wanafunzi wa kike na kwa mwanafunzi wa kiume. Kwa mwanafunzi wa kike adhabu inapaswa kutolewa mikononi, na kwa mtoto mwanafunzi wa kiume ni kwenye Makalio. Pia Waraka huo umeeleza kuwa mwenye Mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko ni Mwalimu Mkuu au Mkuu wa shule husika au Mwalimu mwingine atakayekuwa ameteuliwa tena kwa maandishi.
Pia ametanabaisha kuwa kwa mwanafunzi wa kike Imeelekezwa aadhibiwe na mwalimu wa kike isipokuwa kama shule hiyo haina mwalimu wa kike.
Waziri Kairuki ametoa rai kwa walimu wote nchini wakumbuke kuwa wamekasimiwa Mamlaka
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.