Na. Dennis Gondwe, Ntyuka -DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeshauriwa kuwatafutia viwanja mbadala wananchi walioachia maeneo yao kupisha ujenzi wa Zahanati ya Ntyuka kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
Ushauri huo ulitolewa na kiongozi wa timu namba mbili ya Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Daud Mkhandi alipoongoza kamati hiyo kutembelea na kukagua ukarabati wa Zahanati ya Ntyuka iliyopo Kata ya Ntyuka jijini hapa.
Mkhandi alisema kuwa wananchi wanaodai viwanja ndani ya eneo la zahanati wapewe viwanja mbadala. Vilevile, alishauri ukuta wa zahanati hiyo ufanyiwe skimming na kupigwa rangi.
Akisoma taarifa fupi ya ukarabati wa Zahanati ya Ntyuka Tabibu, Sophia Lusoloja alisema kuwa zahanati iliipokea shilingi 30,817,663 kwa ajili ya ukarabati. “Kazi zilizofanyika ni kuondoa paa la zamani, kupiga kenchi mpya, kuezeka paa jipya, kuweka matungilizi na kupiga plasta sehemu zilizokuwa zimeharibika” alisema Lusoloja.
Ikumbukwe kuwa jiwe la msingi la Zahanati ya Ntyuka liliwekwa na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mheshimiwa John Samwel Malechela tarehe 24 Novemba, 1993.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.