WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Taasisi yake ya Chakula na Lishe imewapatia waandishi wa habari semina yenye lengo la kuwapa ufahamu kuhusu masuala ya lishe ya watoto wachanga na wadogo.
Semina hiyo imefanyika leo jijini Dodoma ikiwa ni mahususi katika Wiki hii ya Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama duniani ambapo Tanzania kama zilivyo nchi zingine inaadhimisha wiki hiyo ambayo hufanyika kila Agosti 1-7 ya kila mwaka.
Akizungumza katika semina hiyo Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Huduma za Lishe wa wizara ya Afya, Grace Moshi amesema maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji hukumbusha umuhimu wa kuboresha hali ya lishe ya watoto kwa kufuata taratibu sahihi za unyonyeshaji maziwa ya mama pamoja na ulishaji wa watoto ili kujenga msingi imara wa Afya na uhai wa watoto ambao ni Taifa la kesho.
Kwa upande wake Afisa Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania, Neema Joshua amesema unyonyeshaji watoto maziwa ya mama hupunguza kiwango cha matumizi ya maziwa na vyakula mbadala vya watoto wachanga na wadogo.
Moshi Amesema lengo la kufanya semina hiyo kwa waandishi wa Habari ni kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kuhusu suala zima la unyonyeshaji wa watoto maziwa ya mama na kuifikisha elimu hiyo katika jamii kupitia vyombo vya Habari.
Chimbuko la Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ni azimio la Innocent la mwaka 1991 ambalo lilikuwa na lengo la kulinda, kuhimiza na kuendeleza unyonyeshaji wa watoto maziwa ya mama ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake kuweza kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua na kuendelea kunyonyesha watoto wao hadi watakapotimiza umri wa miaka miwili au zaidi.
Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘’Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa Afya Bora na ulinzi wa Mazingira’’.
Hapa nchini wiki hii ilizindiliwa rasmi kitaifa Mkoani Tanga katika Halmshauri ya Muheza kwenye Uwanja wa Jitegemee Agost 1,2020 na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi msaidizi Kitengo cha Huduma na Lishe Wizara ya Afya, Grace Mosha akitoa mada mbele ya wana Habari (hawapo pichani).
Neema Joshua, Afisa Mtafiti Mwandamini kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe alipokuwa akitoa mada kwa wanaHabari kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji jiijini Dodoma.
Wanahabari wakishiriki kwenye mafunzo kuhusu Wiki ya Unyonyeshaji iliyofanyika jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.