WATAHINIWA 90,025 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka huu wa 2021 ambao unatarajiwa kuanza leo Mei 3 hadi Mei 21 ukihusisha shule 804.
Mtihani huo unafanyika sambamba na mitihani ya kuhitimu ualimu ambapo jumla ya watahiniwa 6,973 wa vyuo 75 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo kwa ngazi ya stashahada na cheti.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde ameeleza kuwa maandalizi yote yameshakamilika na wamejipanga kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika bila kuwepo udanganyifu.
Amesema kati ya waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita 81,343 ni watahiniwa wa shule na 8,682 wa kujitegemea.
Ngazi ya stashahada waliosajiliwa ni 2,187 ambapo wanaume ni 1,446 sawa na asilimia 66.12 na wanawake wakiwa 741 sawa na asilimia 33.88 wakati ngazi ya cheti waliosajiliwa ni 4,786 wakiwemo wanaume 2,637 na wanawake 2,149.
Dkt. Msonde ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa taratibu zote za uendeshaji mitihani ya taifa zinazingatiwa.
Amesema mitihani ya kidato cha sita ina umuhimu mkubwa kwa kuwa licha ya kupima maarifa, stadi na umahiri wa wanafunzi ndiyo unaowezesha wanafunzi kwenda vyuo vikuu ambako wanazalishwa wataalam.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.