Na.Sifa Stanley, DODOMA
AFISA Tarafa wa Tarafa ya Dodoma Mjini, Zainabu Issah amewahimiza wanafunzi kuendelea kufanya mafunzo kwa vitendo ili waje kuwa viongozi bora hapo baadae.
Aliyasema hayo katika ufunguzi wa mashindano ya mdahalo wa wanafunzi wa shule za Sekondari za Jiji la Dodoma uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.
Afisa Tarafa huyo, alisema ni wakati muafaka kwa wanafunzi kuanza kufanya mafunzo kwa vitendo, hasa kwa kuendesha midahalo ambayo itawajengea hali ya kujiamini na kuja kuwa viongozi bora.
“Kwanza niwapongeze wanafunzi wote mnaoshiriki mdahalo huu hapa mnafanya mafunzo kwa vitendo, na mnajijengea hali ya kujiamini na mtakuja kuwa viongozi bora mnaojiamini baadae, lakini pia niwahimize kuendelea kufanya mafunzo Kwa vitendo ili muendelee kujiimarisha zaidi kitaaluma” alisema Issah.
Akieleza manufaa ya mdahalo huo kwa wanafunzi Pamela George, mwanafunzi wa Shule ya Dodoma Sekondari alisema mdahalo unawasaidia kujenga hali ya kujiamni.
“Kupitia mdahalo huu tunajenga hali ya kujiamini na kuweza kusimama mbele ya watu wengi na kuwasilisha mawazo yetu bila kuwa na woga wa aina yeyote”, alieleza George.
Jumla ya Shule 16 za sekondari zilizopo katika Jiji la Dodoma zinashiriki mashindano ya mdahalo wenye mada isemayo “Je, ukatili wa kijinsia unashusha ufaulu?”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.