Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amewataka wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenda kwenye kata kufanya kazi za jamii ili kupata uzoefu tofauti.
Kauli hiyo aliitoa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kata uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Prof. Mwamfupe alisema “idadi ya wanafunzi wa ‘field’ ni kubwa, waende kwenye kata kufanya kazi za jamii. Wapo waandishi wa habari hapa, habari hazipo kwa Mstahiki Meya na Mkurugenzi pekee, waende kwenye kata. Hii itawanufaisha wao kwa kupata uzoefu na kutakuwa na mafuriko ya habari zinazohusu kata na maendeleo ya wananchi”.
Kwa upande wake Flora Nadoo alisema kuwa kauli ya Mshahiki Meya ni nzuri kwa sababu wanavyoenda kwenye kata wanajifunza vitu vingi na kujua changamoto zinazowakabili wananchi moja kwa moja. “Vile unavyoenda kuona kwa macho na kuja kuandika habari inakuwa na uzito kuliko unapoandika kutoka kwa mzungumzaji” alisema Nadoo.
Nae Emmanuel Lucas alisema kuwa kitendo cha waandishi wa habari wanaojifunza kutoka ofisi kuu ya jiji kwenda kufanya kazi za habari kwenye kata na kuziwasilisha kwa wasimamizi wa halmashauri ni jambo zuri. “Kwa sababu halipo nje ya malengo ya ‘field’ ya kujifunza na kupata uzoefu mbalimbali” Lucas.
Kwa upande wa mwanafunzi wa ‘field’ ya uandshi wa habari, Moureen John alisema “nakubaliana na Mstahiki Meya kwa sababu huko kwenye kata kuna matukio mengi yanayoendelea na sisi hatuyafahamu. Hivyo, tukienda kwenye kata tutapata matukio mengi ya habari za kuwafahamisha wananchi”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.