WANAFUNZI wa Tanzania ni miongoni mwa washiriki wa fainali za mashindano ya kimataifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara yanayoandaliwa na kampuni ya Huawei chini ya kaulimbiu ya "Connectivity, Glory, Future".
Shindano hilo lililozinduliwa jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa njia ya mtandao, mwaka huu limeshirikisha zaidi ya nchi 70 ulimwenguni, na kushindanisha wanafunzi 150,000 kutoka vyuo zaidi ya 2000.
Kwa mwaka jana wanafuzni kutoka Tanzania na Nigeria walikuwa washindi wa jumla katika shindano hilo.
"Kufanya shindano hili la TEHAMA mtandaoni kwa kipindi hiki cha janga la Corona kuna thamani ya kipekee, inaonyesha kwamba Huawei kama waasisi wa miundombinu ya kidigitali Afrika pia tuko makini sana na mkakati wetu wa kuwekeza kwenye vipaji" - amesema Makamu wa Rais wa Huawei Afrika kusini, Liano Yong.
Akiongea pia wakati wa hafla ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Kimataifa ya Elimu ya UNESCO, Ydo Yao, aliipongeza Huawei kwa kuchukua jukumu la mfano la kuunga mkono mipango inayounda, kubuni na kutoa ustadi wa TEHAMA kwa bara la Afrika.
Huawei inatarajia kufundisha zaidi ya wataalamu 700,000 wa TEHAMA ifikapo 2023 Kusini mwa Jangwa la Sahara.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.