Na. Dennis Gondwe, MBABALA
WANAFUNZI wa Kata ya Mbabala katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kulindana dhidi ya ukatili wa kijinsia unaotendeka katika maeneo yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Grace Millinga alipokuwa akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbabala kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.
Millinga aliwataka wanafunzi hao kuwa walinzi wa wanafunzi wenzao dhidi ya kutendewa vitendo vya ukatili. “Wanangu, niwaombe kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie. Ukiona mwenzako kachomwa moto mikono na kufungiwa ndani toeni taarifa kwa walimu au uongozi wa serikali. Ukiona mwenzako ananyanyaswa kimapenzi toa taarifa kwa walimu. Watoto wangu wa kike ukiona unataka kubakwa au mtu anakushikashika toa taarifa kwa mwalimu ili aweze kuchukuliwa hatua. Wanafunzi wote mnatakiwa kupendana ili kwa pamoja mfanikiwe. Huu ndio upendo wenye manufaa” alisema Millinga.
..
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.