WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamekumbushwa kuzingatia masomo yao na kujiepusha na anasa ikiwemo ngono, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya katika umri mdogo ili kufikia ndoto zao na malengo waliyojiwekea katika maisha.
Wito huo umetolewa na mjumbe wa kamati ya kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Jumanne Ngede wakati wa ziara ya kamati hiyo katika shule ya msingi Mtemi Mazengo iliyopo kata ya Ipagala jijini humo.
Akizungumza na wanafunzi hao, Ngede ambaye ni diwani wa kata ya Chamwino aliwataka wanafunzi hususan wa kike kujiepusha na baadhi ya wanaume wenye nia ovu dhidi yao ambao wamekuwa wakiwaingiza katika ngono katika umri mdogo na kuwakatisha masomo kwa kuwapa mimba au magonjwa ya ngono ikiwemo UKIMWI ambao bado ni tatizo katika jamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.