• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wanahabari waombwa kuzingatia weledi

Imewekwa tarehe: December 19th, 2022

MAHAKAMA ya Tanzania hivi karibuni ilikutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari mbalimbali hapa nchini huku Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kwa ujumla kuzingatia utoaji habari sahihi unaozingatia vyanzo muhimu vya habari husika ili taarifa sahihi za Mhimili huo ziwafikie vyema wananchi.

Akizungumza na Wahariri hao kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke-Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Ole Gabriel amesema kuwa, mara nyingi kumekuwa na upotoshaji wa taarifa za Mahakama hali inayosababisha sintofahamu au kuwa na mtazamo hasi wa umma dhidi ya Mhimili huo.

“Tuwe na utamaduni wa kusoma na kufuatilia mageuzi yanayofanyika ndani ya Mahakama ili kuhakikisha kuna ‘story balancing’ ya taarifa tunazotoa kwa umma, bora uchelewe ila utoe taarifa sahihi,” amesema Mtendaji Mkuu.

Ameongeza pia, ni muhimu kuwa na mahusiano mazuri baina ya Mahakama na Vyombo vya Habari ili kuweza kuwafikishia wananchi taarifa muhimu za kimaboresho na vilevile amewataka wananchi kuipa ushirikiano Mahakama hususani katika kipindi hiki ambapo huduma mbalimbali zimeboresha zinaendelea kuboreshwa.

“Ni muhimu wananchi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha haki inatendekea kwa wakati, kwa mfano suala la ushahidi ni jukumu pia la mtu ambaye anaitafuta haki yake kwa sababu yeye ndiye anayejua kwamba uhalisia na tuhuma husika hivyo I muhimu kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka,” amesema Prof. Ole Gabriel.

Aidha, Mtendaji huyo alipata pia fursa wa kuwasilisha Mada ya ‘Mabadiliko ndani ya Mahakama baada ya uhuru hadi sasa’ ambapo amegusia kuhusu historia ya Mahakama pamoja na uboreshaji wa huduma mbalimbali za kimahakama ikiwemo miundombinu ya majengo, matumizi ya TEHAMA, mwenendo wa kiutumishi, Uongozi na rasilimali watu na kadhalika.

“Majengo ya Mahakama katika kipindi cha nyuma yalikuwa duni na sasa yameboreshwa, hii inatokana na kuongezeka kwa idadi ya Mahakama katika ngazi zote; idadi ya Mahakama Kuu kuna vituo 19, divisheni nne (4) za Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi 30, Mahakama za Wilaya 135 na Mahakama za Mwanzo 960, kuanzishwa kwa dhana ya mfumo Jumuishi wa Utoaji Haki (IJC) katika jengo moja katika Mikoa mitano (5) na vilevile ujenzi wa jengo la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania ambalo ni la sita kwa ukubwa duniani,” ameeleza Prof. Ole Gabriel.

Katika wasilisho lake, amebainisha kuwa, Mahakama imepiga hatua katika matumizi ya TEHAMA ambapo kwa sasa mchakato ipo mbioni kupata mfumo wa tafsiri ya Kiswahili na Lugha zingine (hata za asili) kupitia akili bandia (Artificial Intelligence).

Akizungumza na niaba ya Wahariri hao, naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile ameishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kufungua milango na kuweza kukutana nao kwani wameweza kufahamu mambo mengi yanayohusu Mahakama ambayo hawakuyajua awali.

“Tunaishukuru Mahakama kwa kutupa nafasi hii ya kukutana maana si mara nyingi Mahakama inakutana na Vyombo vya Habari, la pili tuwapongeze katika mageuzi tuliyoyashuhudia ya kimiundombinu na kimifumo. Vilevile ni ombi langu kwa baadhi ya mashauri muweze kuyaendesha moja moja ‘live’ ili wananchi washuhudie kama ilivyo kwa wenzetu Kenya,” amesema Bw. Balile.

Mada nyingine zilizotolewa katika Mkutano huo ni pamoja na ‘Uendeshaji wa mashauri katika Mahakama ya Tanzania’ iliyowasilishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Sylivester Kainda na mada ya Maboresho ya Mahakama ya Tanzania ambayo imewasilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.

Katika wasilisho lake, naye, Mhe. Kainda amesisitiza kuhusu matumizi ya TEHAMA kwakuwa yanasaidia katika kuharakisha usikilizaji wa mashauri Mahakamani.

“Sasa hivi Mahakama inauwezo wa kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa katika kipindi husika kwa asilimia mia moja. Kutokana na mafanikio hayo Mahakama imeamua kujenga mfumo mpya “Case Management System” ambao hautaruhusu kabisa matumizi ya karatasi,” amesema Mhe. Kainda.

Akiwasilisha Mada ya Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, kwa upande wake, Mhe. Dkt. Rumisha amesema kuwa jamii inatakiwa kubadili mtazamo hasi kwa Mahakama kwa kuwa imejiboresha katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi, hivyo waone kama ni eneo la kukimbilia.

“Kuna uboreshaji wa huduma mbalimbali za Mahakama umefanyika na tunaendelea zote zinalenga kutoa haki bora kwa mwananchi, mfano katika uboreshaji wa huduma hizo mojawapo tumefanikiwa kupunguza idadi ya hatua/vituo vya ufunguaji mashauri kutoka hatua 38 mwaka 2015 hadi hatua 21 kwa mwaka 2021,” amesisitiza Mhe. Dkt. Rumisha.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na takribani Wahariri 25 pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Mahakama kimelenga kuendeleza ushirikiano baina ya Mahakama na Vyombo vya Habari.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.