Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilifanyika kuanzia tarehe 11 mpaka 20 Oktoba, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha. Kati yao, wanawake walikuwa 16,045,559 na wanaume walikuwa 15,236,772.
Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 572 kulikuwa na muda wa wananchi kuweka pingamizi kwa wananchi waliojiandikisha. Baada ya kushughulikia pingamizi wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikuwa 31,255,303.
Pingamizi za uandikishaji zilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokuwa wakazi wa maeneo husika na wengine kujiandikisha kwenye maeneo wanayofanya shughuli zao za kiuchumi badala ya maeneo yao ya makazi. Aidha, wananchi waliopiga kura siku ya tarehe 27 Novemba, 2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.