• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wananchi Chamwino mfano wa kuigwa, usafi wa J'mosi

Imewekwa tarehe: July 8th, 2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WANANCHI wa Kata ya Chamwino wajitokeza kushiriki usafi wa Mazingira wa kila Jumamosi kwa lengo la kuweka Mazingira safi yanayowazunguka na kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira.

Akiongelea lengo la wananchi wa kata hiyo kufanya usafi wa pamoja wa mazingira, Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa ni kuhakikisha mazingira ya kata hiyo yanakuwa safi. “Kata ya Chamwino, usafi ni tabia yetu. Muitikio wa wananchi kujitokeza kushiriki katika usafi wa pamoja ni mkubwa unaolenga kuweka mazingira safi. Muitikio huo pia ni utekelezaji wa maagizo ya viongozi wetu kuelekeza tufanye usafi wa mazingira ili kujihakikishia mazingira safi na kuepuka magonjwa yanayotokana na uchafu wa mazingira” alisema Nkelege.

Alisema kuwa usafi ulifanyika katika maeneo mbalimbali ukijumuisha usafi wa mitaro ya maji ya mvua, maeneo ya biashara na maeneo ya makazi. “Maeneo haya ni muhimu kwa sababu yanatumiwa na wananchi wengi kupata huduma” aliongeza.

Akiongelea mitaa iliyoshiriki zoezi la usafi katika kata hiyo aliitaja kuwa ni Mtaa wa Mwaja, Mailimbili, Sokoine na Nduka. “Mtaa wa Mwaja usafi wa pamoja ulifanyika katika Shule ya Msingi Chinangali ukihusisha kuzibua na kuondoa mchanga uliofunika mitaro. Pia zoezi la kufyeka vichaka vinavyozunguka eleo la shule ili kuwahakikishia wananfunzi na walimu Mazingira safi na salama.  Kwa Mtaa wa Mailimbili, usafi wa pamoja ulifanyika katika korongo ukihusisha kutoa taka ngumu kama makopo, mifuko ya plastiki na kufyeka vichaka na nyasi zilizoota ndani ya korongo” alisema Nkelege.

Mitaa mingine iliyofanya usafi wa pamoja ni Sokoine na Nduka. “Mtaa wa Sokoine, usafi ulifanyika katika mtaro wa barabara ya Sokoine kuelekea Hoteli ya Okaone ukihusisha kutoa taka ngumu kama makopo na mifuko ya plastiki iliyozagaa ndani ya mtaro. Mtaa wa Nduka usafi wa jumla ulifanyika katika eneo la wazi maarufu kwa Kimbinyiko ukihusisha kufyeka vichaka na nyasi katika eneo hilo” alisema Nkelege.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.