RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 26 Septemba, 2021 amewasili Jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na wananchi wa Jiji la Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, Mawaziri, Wabunge mbalimbali pamojana Madiwani.
Mhe. Rais Samia amewashukuru wananchi wa Jiji la Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kuelelza kuwa mbali na kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia Mkutano huo umemuwezesha kukutana na Marais wenzake na Wakuu wa Taasisi mbalimbali na kuahidiwa kuwa wapo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania katka kuwaletea Wananchi maendeleo.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema katika kipindi cha miezi sita tangu Serikali ya Awamu ya Sita kuingina madarakani idadi ya wawekezaji na wafanyabiashaara wameongezeka kwa kiwango kikubwa hivyo kuchochea kasi ya maendeleo.
Mara baada ya kuwasilli Chamwino, Mhe. Rais Samia amepokewa na wakazi wa Wilaya hiyo ambao walimkaribisha rasmi kama mkazi mwenzao na kumpatia zawadi ya Ng’ombe wa maziwa, kumvika mavazi ya kimila na kumkabidhi Ngao na Mkuki kama ishara ya Kinga na Ulinzi wa Nchi.
Mhe. Rais Samia amewahakikishia wananchi hao kuwa atahakikisha anazitatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na zile zilizoahidiwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Vile vile, Mhe. Rais Samia ameahidi wananchi hao kuwa Serikali itaboresha huduma za jamii ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, ujenzi wa madarasa ya wanafunzi pomaja na Soko la biashara.
Mhe. Rais Samia amewaomba wananchi wa Dodoma wa Watanzania kwa ujumla kuendelea kudumisha amani ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.