Na. Dennis Gondwe, KIKOMBO
WANANCHI wa Kata ya Kikombo wametakiwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya jiji la Dodoma kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Anna Mng’ong’o alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Kikombo kuwahamasisha kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mikopo na walionufaika na mikopo hiyo kuirejesha.
Mng’ong’o alisema “Mama Samia Suluhu Hassan katuangalia sana watu wa chini. Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatoa mikopo ya asilimia 10 katika mapato yake ya ndani kukopesha wananchi. Asilimia nne wanawake, asilimia nne vijana na asilimia mbili ni watu wenye ulemavu. Nipo hapa kuwahamasisha mikopo kwa ajili ya maendeleo. Lakini mkikopa mjitahidi kurejesha ili wananchi wengine wakope. Huo si ndio ustaarabu? Mjitahidi kwanza kuunda vikundi vya watu ambao mnaaminiana na mnaweza kufanya kazi pamoja na kurejesha mikopo mliyokopa”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.