Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI
KATA ya Kikuyu Kaskazini yajivunia maboresho ya huduma za afya kwa kina mama jambo linalopunguza uwezekano wa vifo vya kina mama wajawazito na wakati wa kujifungua katika Zahanati ya Kikuyu.
Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea Zahanati ya Kikuyu kujionea utoaji wa huduma katika jengo la wazazi ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne kwenye Kata ya Kikuyu Kaskazini.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kikuyu, Dkt. Azania Silliah alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, kwa kuwapatia shilingi 33,612,800 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa jengo la wazazi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma aliwapatia shilingi 50,000,000 kwaajili ya umaliziaji wa jengo hilo.
“Napenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Nipende kumshukuru Mbunge wetu, Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kwaajili ya kuhakikisha wazazi wanapata huduma nzuri wakati wa kujifungua kwa kutoa fedha ya uanzishaji wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kikuyu. Pia namshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kuunga mkono jitihada za mbunge wetu” alishukuru Dkt. Silliah.
Mwananchi Johari Issa alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kujenga jengo la wazazi katika Zahanati ya Kikuyu. “Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutujengea jengo la wazazi la kujifungulia pamoja na huduma ya mama na mtoto, kwasababu hapo awali tulikuwa hatuna kabisa jengo la wazazi. Tulikuwa tukitembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma ya kujifungua kutoka sehemu moja kwenda nyingine na tulikuwa tunapata shida kwasababu muda mwingine tunatembea usiku kwaajili ya kufuata huduma. Kwa hivi sasa hatupati tena adha ya kutembea umbali mrefu kwasababu huduma imesogezwa karibu” alishukuru Issa.
Kwa upande wake, Imelda Kessa aliipongeza serikali kwa kuwapelekea vifaa vya kisasa kwaajili ya kujifungulia katika jengo la wazazi. “Naishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutuwekea vifaa vya kisasa, katika zahanati yetu ya Kikuyu. Hii zahanati ni ya mfano kwasababu kuna vifaa na huduma nzuri zinazotolewa hasa wazazi kujifungua. Zahanati ina wauguzi wabobezi katika kazi yao” alipongeza Kessa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.