Na. Josephina Kayugwa, DODOMA
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Sahili Geraruma amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kushiriki vema katika Sensa ya watu na makazi na kutoa taaria zilizo sahihi kwa makalani watakaofika katika maeneo yao kwaajili ya kukusanya taarifa zao.
Aliyasema hayo wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipotembelea mradi wa kilimo wa kikundi cha Kiu ya ufanisi cha vijana ambao wamenufaika na mkopo wa asilimia nne kutoka Halmashauri ya Jiji la Dododma.
“Wananchi mnatakiwa kushiriki vema Agosti 23, 2022. Sensa ni muhimu kwasababu itarahisisha upangaji na kutoa fedha za maendeleo lakini pia utoaji wa huduma za kijamii unategemea idadi ya watu katika eneo husika. Sensa ni kwamaendeleo ya Taifa kwa wale wanaokwenda sehemu zao za kazi wahakikishe wameacha taarifa zao zote muhimu kwa watu ambao watakuwa wamewaacha” alisema Geraruma.
Sambamba na hayo alisema vijana na kina mama wanatakiwa watumie fursa wanazozipata kutoka serikalini ikiwemo mikopo ambayo itawasaidia kujikwamua kimaendeleo.
“Kupitia Sensa Serikali itapata kujua idadi ya watu na kujua kiasi gani kinatakiwa kutolewa kwaaajili ya miundombinu ya kimaendeleo, na kiasi gani cha mkopo kinatakiwa kuwanufaisha wanainchi,” alisema Geraruma.
Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Dodoma ulikimbizwa umbali wa kilomita 129.5 na kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.