Na, Nancy Kivuyo MATUMBULU
SERIKALI ya awamu ya sita inalenga kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wa serikali ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kujenga na kuboresha Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Matumbulu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Matumbulu, Zubery Mbawala alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa waandishi wa habari waliofanya ziara ya kutembelea miradi iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Matumbulu, jijini Dodoma.
Mbawala alisema kuwa ujenzi wa Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Matumbulu ulianza kwa michango ya nguvu za wananchi. “Wananchi walijitolea eneo na wakaanza ujenzi kwa nguvu zao, baadae serikali ndio ikawapokea, kuendeleza ujenzi huo kwa kutoa kiasi cha shilingi 67,000,000 ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika na wananchi wanapata huduma bora. Hata sasa ofisi hii inatumika japo ipo katika hatua za mwisho kukamilika” alisema Mbawala.
Aliongeza kuwa ofisi hiyo kwa miaka minne ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha eneo la utawala bora. Huduma tunazotoa zimeendelea kuistawisha kata yetu hata sasa kuna utulivu, amani na shughuli za maendeleo zinafanywa kwa ufanisi mkubwa sana. Hivyo, tunaishukuru serikali kwa jitihada hizi kubwa za kuhakikisha wananchi wanasogezewa huduma muhimu kwenye maeneo yao” alimalizia Mbawala.
Nae Diwani wa Kata ya Matumbulu, Emmanuel Chibago alisema kuwa kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 serikali imefanya kazi nzuri katika kuwapelekea maendeleo wananchi yanayochochea ushiriki katika uanzishwaji wa miradi ya maendeleo. “Tunawapongeza wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Sio tu ofisi ya kata wameianzisha wao, miradi mingine mingi ni wao ndio waanzilishi, tunawapongeza kwa hilo” alisema Chibago.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.