Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde na Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi leo wameongoza zoezi la usimikaji wa alama ya mpaka katika eneo la Mbuyuni, Kata ya Kizota kuashiria kuanza rasmi kwa zoezi la upimaji na umilikishaji ardhi kwa kaya zaidi ya 8,100.
Zoezi hilo la upimaji litamaliza tatizo lilidumu kwa miaka 30 juu ya uhalali wa makazi ya wananchi katika eneo hilo ambapo awali lilipangiwa matumizi mengine na hivyo nyumba hizo za wananchi kutakiwa kuvunjwa.
Akitoa maelezo ya awali,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Survey Ltd Daud Msungu ameeleza kwamba zoezi la upimaji na utambuzi wa mipaka litaanza mapema leo kwa haraka na weledi mkubwa.
"Namshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kudhihirisha utetezi wake kwa wanyonge ambao kwa takribani miaka 30 hawakuwa na uhakika wa makazi yao katika eneo hili.
Nakushukuru pia Mkurugenzi wa Jiji Ndugu Kunambi kwa utekelezaji wa maagizo na Mhw. Diwani Jamal Ngallya kwa ufuatiliaji. Leo wananchi mtalala kwa amani baada ya kupata uhakika wa umilikishwaji wa maeneo haya" alisema Mavunde.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewataka wananchi wao kuhakikisha wanalipia malipo ya kisheria mapema ili zoezi la kumilikishwa likamilike kiurahisi na kuahidi kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine muhimu sambamba na ujenzi mpya wa Shule ya Msingi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambia akifafanua jambo mbele ya wananchi wa Mbuyuni.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mhe. Anthony Mavunde akiongea na wapiga kura wake baada ya kupata ufumbuzi wa tatizo ambalo limekuwa likiendelea kuwepo kwa zaidi ya miaka 30,
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.