WANANCHI wamehamasika na kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwamo kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali katika wiki ya Uzinduzi wa Sera mpya ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 utakaofanyika kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakati akiwaongoza wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Iseni jijini Dodoma.
Kwa upande wake Balozi wa Mazingira na Mbunge wa Pandani, Mhe. Mariam Omary Saidi aliwataka wakazi wa Dodoma kuhakikisha wanaitunza miti na mazingira ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Awali, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Kanda ya Kati, Mathew Kiondo alihimiza wananchi waitunze miti hiyo baada ya msimu wa mvua kuisha na kudhibiti mifugo.
Alisema si busara kupanda miti leo halafu mwakani tena tunapanda sehemu ile ile ni kupoteza nguvu na fedha za Serikali hivyo alihimiza kuhakikisha miti inapandwa leo.
Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 inatarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Philip Isdor Mpango jijini Dodoma kesho Februari 12, 2022.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.