Na Mwandishi Maalum – Dodoma
WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma wameiomba Serikali kutoa huduma za matibabu ya kibingwa za kuwafuata wananchi mahali walipo mara kwa mara kwa kufanya hivyo wananchi wengi zaidi hasa walioko vijijini watafikiwa na huduma hizo.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dodoma na baadhi ya wananchi waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa taasisi hiyo katika tamasha la Karibu Dodoma festival linalofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma.
Wananchi hao walisema kupatikana kwa huduma hizo katika tamasha hilo kumewafanya wapate nafasi ya kupima afya zao kwa gharama ndogo tofauti na ambavyo wangesafiri na kuzifuata jijini Dar es Salaam.
“Nimefika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) nimepokelewa vizuri nimepimwa uzito, urefu, kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi pamoja na umeme wa moyo, nimepewa dawa za kutumia pamoja na ushauri wa lishe bora kwa afya ya moyo”.
“Ninaiomba Serikali iendelee kutoa huduma kama hizi hasa maeneo yaliyo mbali na Dar es Salaam kwani siyo kila mwananchi anauwezo wa kwenda kupata huduma kama hizi Dar es salaam”, alisema bibi Theresia Duwe mkazi wa maili mbili jijini Dodoma.
“Tunazishukuru taasisi za afya kwa kutusogezea karibu huduma za matibabu ya kibingwa, mimi na wenzangu tumepata huduma za vipimo, ushauri na dawa. ninawaomba wananchi wenzangu watumie nafasi hii kuja katika viwanja hivi kupima na kutambua hali zao”, alishukuru mama Sada Kitenge mkazi wa area c jijini Dodoma.
Kwa upade wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima ambaye alitembelea banda la taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa JKCI alisema Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya zikiwemo za matiba ya kibingwa.
“Ukiangalia idadi ya watu waliojitokeza kupima pamoja na matatizo ya moyo waliyokutwa nayo kuna haja ya Serikali kutoa elimu ya kutosha ya jinsi ya kuepukana magojwa haya pamoja na kuhakikisha wale wanaokutwa na matatizo mara baada ya kufanyiwa upimaji wanapata dawa za kutumia”, alisema Dkt. Gwajima.
Huduma zinazotolewa katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ni upimaji wa urefu na uzito, kiwago cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu (BP), kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography), kipimo cha mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography), kutoa dawa kwa watu watakaokutwa na matatizo ya moyo na rufaa ya moja kwa moja ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi katika taasisi hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akiangalia dawa za moyo zinazotolewa bila malipo na kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya Sun Pharmaceutical Industries Ltd. Kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo ya moyo waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa taasisi hiyo katika tamasha la Karibu Dodoma festival linalofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma.
Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwahudumia wananchi waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa taasisi hiyo katika tamasha la Karibu Dodoma festival linalofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma.
Mwakilishi wa kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu ya Sun Pharmaceutical Industries Ltd. Bruno Mlowe akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa za moyo kwa wananchi waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa taasisi hiyo katika tamasha la Karibu Dodoma festival linalofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.