WAKAZI wa Manispaa ya Dodoma wameshauriwa kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Madiwani ili kupata taarifa za miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Manispaa yao na kujua kazi inayofanywa na Madiwani waliowachagua.
Wito huo umetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede kuelekea Mkutano wa Baraza hilo wa kisheria kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/18 utakaopokea taarifa mbalimbali za Manispaa hiyo kitakachonyika Oktoba 31 mwaka huu katika ukumbi wa Manispaa.
Naibu Meya Ngede alitoa wito huo wakati alipoongoza Mkutano wa awali wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo lililopokea taarifa za utekelezaji wa miradi kutoka katika Kata zote 41 za Manispaa ya Dodoma Oktoba 25 mwaka huu.
Aliiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuongeza matangazo kwa wananchi kuhusu tarehe ya Mkutano huo ili waweze kuhudhuria kutokana na umuhimu wa mkutano huo ambao ni wa wazi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.