Wakazi wa maeneo tofauti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wamezungumzia hali ya usafi katika Jiji hilo huku wakipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji katika uboreshaji wa hali ya usafi katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza na Dodoma City Tv mkazi wa mtaa wa Barabara ya nane Ramadhani Mussa amesema Halmashauri ya Jiji imepiga hatua kubwa katika suala la usafi ukilinganisha na ilivyokua awali, ambapo hali haikuwa nzuri katika baadhi ya maeneo mfano barabara, masoko na vituo vya usafiri.
“kiukweli Jiji limepiga hatua nzuri, tunaona maendeleo makubwa kwenye upande wa usafi, tunawapongeza watu wa mazingira wanafanya kazi kubwa sana, barabara zinafagiliwa kila siku asubuhi yaani jiji linang’aa” – Alisema Mussa.
Kwa upande wake Edson Magaya mkazi wa Maili mbili amesema kuwa anafurahishwa na uwepo wa magari mengi ya taka yanayofanya kazi ya kubeba taka kutoka kwenye maeneo ya kukusanyia taka na kuzipeleka nje ya mji kwenye dampo na kuuacha mji ukiwa katika hali ya usafi.
Magaya pia amelipongeza Jiji la Dodoma kwa kuweka vitunzia taka kwenye kila eneo, hasa maeneo yenye mikusanyiko kama vile masoko, vituo vya daladala, vituo vya Afya, mashule pamoja na Vyuo.
“Siku hizi anaetupa taka hovyo, ni haki kuadhibiwa kwasababu atakua amefanya makusudi, kwasababu kila kona kuna vitupia taka kwa hiyo mtu utakosa sababu ya kutupa taka hovyo, kiukweli jiji linapendeza na mabadiliko tunayaona” aliongeza Magaya.
Ramadhani Mussa mkazi wa Barabara ya nane jijini Dodoma akizungumza na mwandishi wetu juu ya hali ya usafi Jijini Dodoma.
Mkazi wa Maili mbili Edson Magaya alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu kuhusu hali ya usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.