Na. Sizah Kangalawe DODOMA RS - Habari
KATIBU Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya ameongoza kikao cha kamati ya lishe robo ya kwanza (Julai -Septemba 2024) kujadili utekelezaji wa viashiria vya Mkataba wa Lishe.
Kikao kazi hicho kimefanyika Oktoba 23,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau na mashirika yanayojihusisha na lishe kutoa elimu kwa Wananchi ili kuepukana na desturi za kuamini katika chakula cha aina moja.
"Kuna mila na desturi zipo kule, wao wanaamini kwenye chakula kimoja na wanaona ufahari juu ya chakula chao, na hiyo ndio inapelekea wakati mwingine kukosa virutubisho vya muhimu kwenye miili yao.
"Ni msisitizo wangu kwa wadau wote mliopo hapa nendeni mkalifanyie kazi suala hili, angalieni mitazamo ya watu ambayo inaendana na mazingira ya mila na desturi zilizopo na tuangalie jinsi gani ya kuwafanya wao kuwa na mtazamo chanya juu ya lishe ili tupate matokeo makubwa", Amesema Katibu tawala Mmuya.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha Maafisa lishe ngazi ya Mkoa, Wadau wa lishe kutoka mashirika mbalimbali, viongozi wa Dini pamoja na wajumbe kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.