Na Carine Abraham Senguji, Dodoma
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) inashiriki kambi maalum ya matibabu ya kibingwa inayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC) kuanzia Julai 15-25, 2024.
Katika kambi hiyo wananchi wamejitokeza kwa wingi na kushukuru kwa huduma nzuri za kibingwa walizopatiwa na madaktari wa BMH.
Mary Penda ni mmoja wa wananchi waliojitokeza kupata huduma za uchunguzi kutoka kwa madaktari wa BMH na kushukuru kwa huduma nzuri.
"Mimi hapa nimemleta mama yangu kupata huduma na nimefurahishwa sana na huduma niliyopata katika banda la BMH kwani huduma ni nzuri na wahudumu ni wakarimu sana," amesema Bi. Mary.
Penda ameendelea kwa kuipongeza BMH kwani siku zote wanatoa huduma nzuri hata katika Hospitali yao.
"Kwakweli naishukuru sana BMH nimefika mara kadhaa kupata huduma pale na huduma zao ni za viwango vya hali ya juu," ameongeza Bi. Mary.
Katika hatua nyingine Amani Petro ameishukuru mkoa wetu wa Dodoma na kuwakutanisha na Madaktari bingwa kwaajili ya uchunguzi.
"Naishukuru serikali yetu kwa kufanya kambi ya uchunguzi wa matibabu bure kwani itasaidia wananchi kujua afya zao hivyo natoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi," ameeleza Bw. Amani.
Dkt. Baraka Alphonce ambae ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na mmoja wa washiriki kutoka BMH amesema kuwa katika kambi hii BMH itatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo na magonjwa ya ndani kwa wananchi wote watakaofika kupata huduma.
"Tumekujana na vipimo vya uchunguzi wa magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kisukari hivyo tunaomba Watanzania kufika kwa wingi kwaajili ya kufanya uchunguzi huu ambao ni bure kabisa," amesema Dkt. Baraka.
Hata hivyo Dkt. Baraka ameiomba Ofisi ya Mkoa kutangaza huduma hii kwa ukubwa ili watu wajitokeze kwa wingi kuja kujua afya zao
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.