WANANCHI wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kufika kwenye maonesho ya Sherehe za Nanenane Kanda ya Kati Kitaifa 2024 ili wachukue teknolojia zinazooshwa na wataalam wa kilimo na ufungaji ili kuwawezesha kukima na kufuga kwa tija.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Prof. Riziki Shemdoe alipotembelea Mabanda ya Taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na shughuli za Kilimo, Mifugo na uvuvi kwenye viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
“Tumieni siku hizi nane za maonesho haya kuja kuchukua teknolojia kwenye maonesho haya. Mtu akifika hapa ataondoka na kitu, hapa watakuja watu kutoka Mataifa mbali mbali hivyo sisi wenyeji tunapaswa kuwa mstari wa mbele” Amesema Prof. Shemdoe.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri aliyeambatana na Katibu Mkuu huyo, alisema wakulima na wafugaji wakienda kufanyia kazi teknolojia hiyo hata kwa asilimia 40 tu, wataweza kubadilisha maisha yao pamoja na uchumi na kuifanya Tanzania kuwa Kapu la chakula la Afrika kama ilivyo dhamira ya Mhe. Rais.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.