WAKAZI wa Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma walipewa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na malezi bora ambayo imetolewa katika Ofisi ya Afisa Mtaa wa Mwaja kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua yanayoendelea kwenye jamii.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Mratibu wa Jinsia na Watoto, Fatuma Kitojo amewataka wazazi hao kuwa walezi bora kwa watoto wao na kutowatamkia maneno mabaya ambayo yanawakatili kisaikolojia ili wakubalike na jamii inayo wazunguka.
Kitojo alisema kuwa ni muhimu kwa wazazi kuelewa kwamba maneno wanayosema yanaweza kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya watoto kihisia, kujitambua, na uhusiano mzuri na Watoto wengine.
“Watoto wetu wanatupenda sana na wanapenda kuona sisi tunafanikiwa ni kweli tuna shughuli nyingi tunakimbizana na muda na maisha kwa sababu za hali za kiuchumi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. lakini tunajua kwa asili mwanamke ndiyo mlezi namba moja. Kwahiyo tunatakiwa tutenge mda wa kuzungumza na watoto wetu” alisema Kijoto.
Naye, Afisa Mradi wa Ahadi, Elizabeth Kahabi amefafanua kuhusu mradi wa AHADI ambao upo chini ya shirika la World Vision na unatekelezwa na wadau kutoka shirika la TAHEA kwa lengo la kuwasaidia vijana kiuchumi, kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia na afya ya uzazi.
“Mradi huu unahusiana na vijana lika barehe wenye umri chini ya miaka 10 hadi 24. Tumekuja leo hapa kuwajengea uwezo na kuwapa elimu wakazi wa Chamwino wawasaidie vijana kujiunga na taasisi yetu kwa sababu kuna mambo mazuri na yakufundisha wawaruhusu hawa ambao hawasomi maana ndiyo tumeanza nao. Lakini mara nyingi tunatumia vijana wenye kuwapa taarifa wenzao kwa kuwa na viongozi katika makundi” alisema Kahabi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.