WANASAYANSI wameonya kuwa ziwa la Lava linajaa kwa kiwango cha kutisha juu ya Mlima wa Volcano wa Nyiragongo uliopo juu ya mji wa Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Januari, mwaka 2002, lava ilimwagika kutoka mlima huo kwa kasi hadi katika mji wa Goma na kusababisha vifo vya watu 250 na kuharibu asilimia 20 ya mji huo.
Kikundi cha wanasayansi wanaochunguza matukio ya milima, wameonya kuwa mwamba unaoyeyuka unaweza kulipuka tena kupitia kuta za ziwa la volkano.
“Sasa, hali inaonesha dalili za kutokea volkano nyingine,” alisema mtaalamu wa volkano na Milima Dario Tedesco, katika mahojiano yaliyofanyika kwenye jarida la masuala ya kisayansi.
Tathmini yao inaonesha kuwa hatari kubwa zaidi ya mlima huo itatokea katika kipindi cha miaka minne, ingawa wanaamini tetemeko la ardhi linaweza kusababisha mlipuko huo mapema.
“Hii ni volkano hatari zaidi duniani! Profesa Tedesco aliongeza. Watu takribani milioni moja wanaishi katika mji wa Goma.
Chanzo: HabariLeo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.