Na. Theresia Nkwanga, MNADANI
WANAUME wa Kata ya Mnadani wametakiwa kuachana na kisingizio cha mgawanyo wa majukumu na kushirikiana na wanawake katika malezi na makuzi ya watoto ili kukabiliana na janga la ukatili wa kijinsia ambalo kwa kiasi kikubwa linawaathiri wa watoto.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Viti Maalum wa Jiji la Dodoma, Rosemary Nitwa alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Mnadani iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Nitwa alisema kuwa dunia imeharibika sana niwajibu wa wazazi pande zote kushiriki katika malezi ya watoto na kuachana na kasumba ya kuwaachia malezi ya watoto wanawake pekee, ili kuwapa watoto malezi bora na kuwalinda dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“Nafurahi kuwaona wanaume wengi hapa kuliko kina mama wanaume mmekuwa nyuma sana katika malezi ya watoto, suala hili halikubaliki kila mwanaume anayezaa na mwanamke anapaswa kuwajibika katika malezi ya mtoto wake. Niwaombe sana msikwepe majukumu yenu tusaidiane kwenye malezi hawa watoto ni wetu sote tupunguze sababu ya mgawanyo wa majukumu. Watoto wetu wanafanyiwa vitendo vya ukatili kwa kukosa ulinzi kutoka kwa sisi wazazi kwa kuwa tupo bize na utafutaji wa pesa, utajisikiaje unapata pesa lakini mtoto wako ni shoga au msagaji mtoto anapoharibika ni hasara kwa wazazi wake wote. Tuwalinde watoto wetu tukiacha wakaharibika tunatengeneza Taifa gani la kesho” alisema Nitwa.
Akielezea alisema kuwa ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu yeyote mwanamke au mwanaume kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi. Hivyo, tunapaswa kutoa taarifa pindi tunapofanyiwa au kushuhudia aina yoyote ya ukatili.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.