WAJUMBE wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuchangua viongozi wenye uwezo wa kuongoza na kuleta maendeleo tofauti na kuchagua kwa kuangalia sura.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asha Vuai alipokuwa akifungua mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Vuai alisema “niwasihi ndugu zangu tutumie nafasi hii kuchagua viongozi watakaotuunganisha kama wanawake kwa kutumia changamoto zetu ili ziweze kutatuliwa. Pia viongozi hao wawe kichocheo cha kutupatia fursa za kiuchumi zinazopatikana. Hivyo, tuchague viongozi kwa sifa zao siyo sura zao” alisema Vuai.
Mkuu huyo wa idara alisema kuwa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi linalenga kuondoa matabaka na sheria kandamizi ambazo zitasaidia kuondoa ubaguzi wa kiuchumi. “Kwa wanawake ni jambo muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa na pato la taifa kwa ujumba. Ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi ni kichocheo kizuri cha maendeleo ya nchi yetu na jamii kwa ujumla. Kwa sabau ushiriki wa wanawake katika uchumi unaleta mabadiliko makubwa sana katika familia na jamii kwa ujumla” alisema Vuai.
Katika uchaguzi huo nafasi zilizowaniwa ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, katibu msaidizi na mweka hazina ikiwa ni maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.