Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) imetangaza kuanza kwa matumizi ya Tiketi za Kieletroniki kwenye mabasi yanayokwenda mikoani na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo wametakiwa kusitisha utoaji huduma kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katika taarifa yake Mamlaka imewaagiza wasafirishaji wote wa abiria kwa mabasi kuzingatia masharti ya leseni za usafirishaji na matakwa ya kanuni za leseni za usafirishaji – Magari ya Abiria zilizotangazwa kwa tangazo Na. 76 kwenye gazeti la Serikali Februari 7, 2020.
Maamuzi haya yanasimamiwa na Kanuni ya 4 (2) (c); Leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka.
Pia, Kanuni ya 24 (b) (d); Msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za kielektroniki kwa abiria.
Mamlaka imewataka wasafirishaji watoe tiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza. Hivyo basi kuanzia tarehe 6 Januari, 2021 hakuna msafirishaji atakayeruhusiwa kusafirisha abiria bila kutoa tiketi za kielektroniki kwa abiria wote katika njia zifuatazo:
Dar es Salaam – Tanga
Tanga – Arusha
Dar es Salaam – Lindi
Dar es Salaam – Mtwara
Dar es Salaam – Iringa
Dar es Salaam – Njombe
Dar es Salaam – Ruvuma
Dar es Salaam – Mbeya
Dar es Salaam – Tunduma
Dar es Salaam – Rukwa
Dar es Salaam – Morogoro
Dar es Salaam – Kilombero
Dar es Salaam – Ifakara
Dar es Salaam – Malinyi
Dar es Salaam – Mahenge
LATRA imesema katika taarifa yake kuwa, kupitia mfumo huu, Wananchi watatumia simu kukata tiketi jambo litakaloepusha wizi, ulanguzi wa tiketi na adha za wapiga debe. Vilevile, unalenga kukomesha vitendo vya upandishaji holela wa nauli hasa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.