WASAJILI wa mfumo wa usajili wa wafanyabiashara ndogondogo wametakiwa kuwa waadilifu katika utoaji wa vitambulisho kwa kuwapatia wale ambao wanastahili.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Biashara
na Maafisa TEHAMA ngazi ya mikoa kuhusu utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo nchini.
Waziri Dkt. Gwajima amewaagiza wataalamu hao kuhakikisha wanakwenda kutoa elimu waliyoipata kwa wataalamu ngazi ya wilaya na kata na kufanya kazi kwa kushirikiana baina yao kwa sababu mfumo
umetengenezwa kila mmoja kushiriki.
“Tunachofanya hapa ni kutekeleza maelekezo ya mhe Rais yenye lengo la kuwasaidia wafanya biashara wadogo hivyo usajili unatakiwa kufanyika haraka ili suala la utoaji mikopo lianze” amesema Dkt. Gwajima.
Ameongeza kwamba mafunzo hayo yanayolenga kuchochea maendeleo ya wafanyabiashara ndogondogo nchini ambayo ni ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba, wafanya biashara ndogondogo
watambulikwe na waunganishwe na mifumo ya fursa za kiuchumi.
“Ni imani yangu kuwa sote tutakuwa tayari kutekeleza jukumu hili muhimu mara tu baada ya kupata mafunzo haya ikiwa ni kwenda kusimamia na kutoa mafunzo kwa Maafisa Biashara, Maafisa
Maendeleo ya Jamii na Maafisa TEHAMA katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye mikoa yenu. Hivyo, kufanikiwa kwa zoezi la utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho kwa
wafanyabiashara ndogondogo nchini kutategemea juhudi zenu za kujituma katika kutoa mafunzo, kusimamia zoezi hilo kwa karibu pamoja na kushirikiana na Maafisa hao kufuatilia kila hatua ili kufikia lengo
lililokusudiwa.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.