NAIBU katibu Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI) Sospeter Mtwale wamewataka washiriki wa Bonanza la Michezo Jijini Dodoma kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara na sio kusubiri tu wakati wa bonanza.
Mtwale amebainisha hayo katika Bonanza la michezo lilofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin Jijini Dodoma ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Ameeleza kuwa mazoezi huimarisha afya ya akili na mwili na kuepusha magonjwa hasa nyemelezi.
"Kama nilivyosema awali michezo ni afya, michezo inatusaidia kupambana na magonjwa hususani magonjwa nyemelezi lakini pia tunaimarisha afya ya akili kwahiyo tuwe na mazoea ya kufanya mzoezi mara kwa mara tusisubiri matukio kama haya " Amesema Mtwale
Sambamba na rai hiyo Mtwale ametoa wito kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendeleza tamasha hili la michezo akibainisha kuwa pamoja na ushindani washiriki hupata fursa ya kukutana na watu mbalimbali nje ya maeneo yao ya kiutendaji.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dtk. Fatuma Mganga ametoa wito kwa Mikoa na Halmashauri nchini kuandaa matamasha ya michezo akisisitiza kuwa michezo huimarisha utendaji kazi.
Kwa upande wake mratibu wa Michezo kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Mbijima amebainisha kuwa pamoja na kushiriki bonanza hili washiriki walipata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa huduma za afya.
"Tunatarajia kuongeza michezo mingine kwa bonanza lijalo ili kila mmoja apate fursa ya kushiriki bonanza hilo" Amehitimisha Mbijima.
Washiriki wa Bonanza hilo ni taasisi mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Muungano Jogging Club pamoja na Dodoma Sports Club.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.