• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wasimamizi wa Mikopo Halmashauri Wapewa Mafunzo

Imewekwa tarehe: December 7th, 2024

Na. Coletha Charles, DODOMA

Kamati ya huduma ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu ngazi ya halmashauri wamepewa mafunzo ya kuhakiki, kutathimini, sheria na kanuni za utoaji wa mkopo ili kuwajengea uwezo wa usimamizi wa mikopo hiyo.

Mafunzo hayo yalitolewa katika Ofisi ya Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kutoa muongozo wa utoaji na usimamizi wa mikopo kwa wasimamizi hao. Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, Charity Sichona alisema kulingana na kanuni mpya za mwaka 2024 wameweka ratiba ya kufanya tathimini ya maombi ya kikundi kwa kuweka kumbukumbu.

Alisema katika ngazi ya kata wasimamizi wameendelea kutoa mafunzo na kusajili vikundi. Alisema kuwa takribani vikundi 1,000 vimejisajili na hatua ya kuomba mkopo inaendelea kwa kuangalia tathimini ya miradi ya wanakikundi. “Mafunzo kama haya tulishatoa katika ngazi mbalimbali hasa kata ambapo wanajukumu kubwa la kuchakata maombi hayo na kuwapatia mafunzo wanakikundi hadi hatua ya kupata mikopo. Lakini pia mafunzo kama haya yanaweza kujenga uelewa mpana zaidi kwa viongozi ngazi ya halmashauri” alisema Sichona.

Mwezeshaji wa Mafunzo, Daniel Mpangwa alisema kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa makundi ambapo wanawake kuanzia watu wa tano 40%, vijana kuanzia wa tano 40% na watu wenye ulemavu 20% kuanzia watu wawili au mmoja.

Alisema kuwa wasimamizi wanatakiwa kuzingatia mfumo jumuishi na mfumo wa serikali ulioboresha kwa maelekezo kama utoaji wa mikopo kwa utaratibu wa taasisi za fedha, majukumu ya taasisi ya fedha na mamlaka ya serikali za mitaa, tathimini na uboreshaji, mikopo ya vifaa, ushirikiano na wadau mbalimbali na kuepuka mgongano wa kimaslahi. “Naamini kamati hii ikitoka hapa itaenda kufanya kazi vizuri na kwa weledi. Lakini, mafunzo haya yameweza kutolewa ngazi nyingine za kamati za maendeleo za kata ambayo tayari yamekwishafanyika lakini pia kwa Afisa Maendeleo Kata ambapo sasa michakato ya mikopo bado inaendelea” alisema Mpangwa.

Mratibu wa Mikopo ya asilimia 10 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hidaya Mizega alisema kwa mujibu wa sheria ya utengaji wa fedha za mikopo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zitazingatia uwiano wa 4:4:2 wa waombaji wote wa mkopo bila ya kumpendelea yeyote.Serikali za Mitaa zitaruhusiwa kuhamisha fedha na kutumika katika kundi lingine lenye uhitaji kulingana na wingi wa watu kwa maelezo juu ya wajibu wa mamlaka ya utengaji, utoaji na urejeshaji wa mikopo, aliongeza.

Viwango vya ukomo wa utoaji wa mikopo midogo ni shilingi 500,000 kiwango cha chini na kiwango cha juu ni shilingi 9,999,999. Mkopo wa kati kiwango cha chini ni shilingi 10,000,000 na kiwango cha juu ni shilingi 49,999,999 na mkopo mkubwa kiwango cha chini ni shilingi 50,000,000 na kiwango cha juu ni shilingi 150,000,000.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.