VIONGOZI wa sekta za afya Nchini wametakiwa kuwaruhusu Wataalamu wa Maabara kushiriki kwenye Makongamano kwa mustakabali wa kuboresha utoaji huduma ya afya kwa Wananchi kwani taaluma hiyo ina thamani kubwa Nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko wakati akifungua rasmi Kongamano la 37 la Wataalamu wa Maabara ambapo amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
“Kumekua na tabia ya viongozi kutowaruhusu wataalamu hawa kuhudhuria Makongamano, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa taaluma yao hivyo, kupitia Kongamano hili, nawataka viongozi wawaruhusu wataalamu hawa kushiriki na kusiwe na uzembe kwenye hili.” Amesema Dkt. Biteko
Naye, Waziri mwenye dhamana ya sekta ya afya Mhe. Jenista Mhagama, amesema Serikali imefanya maboresho kwenye sekta hiyo kwa kuongeza mashine za kiuchunguzi.
“Mhe Rais amefanya uboreshaji wa mashine za kiuchunguzi kama MRI, Ex–ray, Ultra sound na kuhakikisha huduma zinazotolewa na wataalamu hawa zinaendana na uboreshaji huu hivyo kupunguza wagonjwa wanaohitaji kwenda kupata matibabu nje ya nchi” Amesema Mhe. Mhagama
Aidha, akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule katika salamu zake amesema kipindi cha Serikali ya awamu ya sita kimeinufaisha Dodoma katika sekta ya afya.
“Dodoma tunavyo vituo vya kutolea huduma za afya 516, vituo vya kutolea huduma za maabara 217. Nitoe pongezi nyingi kwa Mhe. Rais kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na dawa kwa kiasi kikubwa kwani ametoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 18.3 kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba na dawa” Mhe. Senyamule.
Akisoma risala ya Chama cha wataalamu wa Maabara za AfyaTanzania (MeLSAT), Rais wa chama hicho Bw. Yahya Mnung’a, ametaja changamoto ya utofauti wa mitaala ya kufundishia baina ya vyuo vya afya kuwa inazalisha wataalamu wa Maabara wasio na ufanisi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.