OR-TAMISEMI
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imehitimisha mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa masuala ya kijamii na Mazingira kwa watumishi wa Halmashauri 12 zinazotekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa TACTIC unaotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya Dunia.
Akizungumzia mafunzo hayo, Mratibu wa Mradi wa TACTIC kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Emmanuel Manyanga amesema tayari miradi imeshaanza kutekelezwa kwenye Miji 12 ya awamu kati ya Miji 45 na lengo la kuwaita wataalamu hao ni kuwaandaa kuwa sehemu ya usimamizi wa mradi katika kusimamia masuala ya utunzaji wa mazingira athari za kijamii.
“Tumezungumza na hawa wataalamu kuhusu utunzaji wa mazingira na kutokuharibu mazingira wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi wa mradi ili kutunza mandhari ya miji na katika masuala ya kijamii tumeangalia zile changamoto ambazo wanakutananazo wananchi kama mafuriko ,kujaza vifusi barabarani,kuziba barabara mambo kama hayo hatutaki yawepo kabisa” amesema Mhandisi Manyanga
Nao, baadhi ya washiriki akiwamo Mtaalamu mshauri UNITEC na mkandarasi Dkt. Fatma Waziri, Mtaalamu wa masuala ya kijamii Jiji la Dodoma, Mufungo Manyama na Mtaalamu wa masuala ya Mazingira kutoka Jiji la Mwanza, Desderius Polle, wamesema mafunzo hayo yametoa mwanga wa kukabiliana na majanga na athari za kijamii na mazingira wakati wa utekelezaji wa mradi wa uendelezaji miji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.