Na. Faraja Mbise, DODOMA
Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetakiwa kuwajengea uwezo wa kimbinu na kuwatumia wataalam wa ndani ili kuongeza mapato ya ndani sambamba na kubuni miradi ya kimkakati yenye tija kwa maendeleo ya nchi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akizungumza na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, waliotembelea Dodoma kwa lengo la kujifunza na kuongeza wigo wa namna sahihi ya kuongeza mapato ya ndani kupitia miradi mbalimbali, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Hakuna mapato madogo na hakuna mradi mdogo, ila tunapoandaa miradi, tujiulize tunaandaa miradi yenye mfumo gani?. Kwahiyo, tunavyofikiri miradi, hata yenye mtazamo wa kibiashara lazima tufikirie kwenye kukua kwake. Hivyo, kila kitu kinaweza kikaanza kwenye udogo, kikakua na mapato yaleyale madogo tunaweza tukaanzisha miradi kwa mapato ya ndani. Nilichokuwa nataka kusema cha kwanza ni kutumia wataalam ili kutuongoza katika namna bora ya kutekeleza miradi hiyo” alisema Dkt. Sagamiko.
Akizungumza kuhusu ziara ya Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, aliwataka watumie fursa hiyo ya ziara ili kuongeza nguvu katika kutekeleza miradi. “Naomba ziara hii itumike kuwajenga, kuwaongezea nguvu zaidi, kwamba tulipo tunaweza kufanya pakubwa zaidi badala ya kuwakatisha tamaa, ni kweli tumekuja kujifunza miradi. Lakini kikubwa tumekuja kutanua fikra zetu, tupate matamanio ya mambo ya kwenda kufanya Kyerwa, kikubwa tumekuja kupanua wigo” alisisitiza Dkt. Sagamiko kwa kauli ya kutia moyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.