WATAHINIWA wa Kidato cha Sita 113,504 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2024 ambapo kati yao Watahiniwa wa Shule ni 104,449 na Watahiniwa wa Kujitegemea ni 9,055.
Kati ya Watahiniwa wa Shule 104,449 waliosajiliwa, wavulana ni 57,378 sawa na asilimia 54.9 na wasichana ni 47,071 sawa na asilimia 45.1.
Aidha, watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 232 ambapo kati yao 201 ni wenye uoni hafifu,16 ni wasioona na 15 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili. Kati ya Watahiniwa wa Kujitegemea 9,055 waliosajiliwa, wavulana ni 5,515 sawa na asilimia 60.91 na wasichana ni 3,540 sawa na asilimia 39.09. Aidha, Watahiniwa wa Kujitegemea wenye mahitaji maalum wako 3 ambapo wote ni wenye uoni hafifu.
Mwaka 2023 idadi ya watahiniwa wa Shule na Kujitegemea waliosajiliwa walikuwa 106,883 hivyo kuna ongezeko la jumla ya watahiniwa 6,621 (6.19%) kwa mwaka 2024 ukilinganisha na mwaka 2023.
Mitihani ya Kidato cha Sita (ACSEE) na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada itaanza rasmi tarehe 06 Mei, 2024 Tanzania Bara na Zanzibar. Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) utamalizika kufanyika tarehe 24 Mei, 2024 na Ualimu tarehe 20 Mei, 2024.
Mtihani wa Kidato cha Sita utafanyika katika jumla ya shule za Sekondari 931 na Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 258. Aidha, Mtihani wa Ualimu utafanyika katika Vyuo vya Ualimu 99.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.