WATANZANIA wapatao milioni 29 wanatarajia kupiga kura kesho tarehe 28 Oktoba, 2020 katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jumla ya Wapiga kura 29,188,348 wameandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Wapiga kura 566,352 wameandikishwa katika Daftari la Wapiga kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Da es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema katika uchaguzi huu kuna vituo vya kupigia kura vipatavyo 81,567 vikiwemo vituo 80,155 vinavyokana na Daftari la Kudumu la Wapiga kura NEC na vituo 1,412 vinavyotokana na Daftari la Wapiga kura la ZEC.
Vilevile amesema kuwa vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu vinashiriki ambapo kwa mujibu wa takwimu kuna jumla ya wagombea 1,257 katika nafasi za ubunge na jumla ya wagombea 9,237 katika nafasi za udiwani.
Jaji Kaijage amesema kuwa vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.