WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewaasa Watanzania kuheshimu, kuthamini na kujivunia utamaduni wa jamii zao.
Pindi Chana amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Holi Milan 2023 la kusherehekea miaka 75 ya Uhuru wa India, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wa India kwa kutumiza miaka 75 ya Uhuru wao.
"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na India uliodumu tangu uhuru ili kuhakikisha kuwa, shughuli za Utamaduni na Sanaa baina ya nchi hizi mbili zinaendelea kukua na kuwa chanzo cha mapato kwa wananchi wa Mataifa yetu mawili"
Balozi Dkt. Pindi ameeleza kuwa tamasha hilo linafundisha watu kuheshimu na kuthamini Utamaduni wao akiwaasa Watanzania na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wapende na wajivunie utamaduni wao ambao umekua chanzo kikubwa cha kuleta mabadiliko chanya ya kupenda kufanya kazi na kushirikiana na watu mbalimbali.
"Tanzania na India tumekua na ushirikiano wa miaka mingi, tumeshuhudia nchi zetu zikishirikiana katika masuala mbalimbali ya afya, elimu, utamaduni, michezo na biashara.
Aidha, Balozi Dkt. Pindi Chana ameupongeza Ubalozi wa India kwa kuandaa tukio hilo muhimu hapa nchini akisisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji.
Tamasha hilo limehudhuriwa na mabalozi na viongozi mbalimbali na kupambwa na burudani, Sanaa na Utamaduni wa Tanzania na India wenye kuonesha hostoria ya Mataifa hayo mawili.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.