RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendelea kuenzi mashujaa kwa kudumisha amani na kusisitiza kuwa Tanzania ni moja na haitagawanyika.
Rais Dkt.Samia alibainisha hayo Jijini Dodoma katika Maadhimisho siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambapo amesema ni muhimu kuenzi mashujaa kwa kudumisha amani ,Umoja na mshikamano.
Aidha, Rais Dkt. Samia aliagiza mnara wa mashujaa unaoendelea kujengwa katika mji wa Serikali Mtumba katika utekelezaji wa agizo alilolitoa Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa 2022 ukamilike kwa wakati huku akiagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha kwa wakati.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama alisema mnara wa mashujaa wenye zaidi ya mita 100 utajengwa huku agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan la kujengwa mnara wa Mashujaa likitekelezwa.
Halikadhalika, Mhagama aliipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya kujengwa mnara wenye hadhi ya Makao makuu ya nchi Dodoma katika mji wa Serikali .
Kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka Tanzania imetenga siku maalum ya kumbukizi ya Mashujaa waliojitoa kulipigania Taifa la Tanzania wengine hata kupoteza maisha yao na hii ni kama ishara ya kukumbuka uzalendo , Ujasiri na ushujaa waliouonesha .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.