Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Barthazar Ngowi (pichani aliyesimama) amewakumbusha Maafisa Watendaji Kata wa Jiji la Dodoma kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inataka matokeo ya kazi.
“Serikali hii inataka kumfanya mtumishi apimwe kulingana na matokeo ya kazi. Lazima tutumie vizuri muda na mishahara tunayolipwa, kwa kufanya kazi na kutoa matokeo chanya” amesisitiza Ngowi.
Ngowi ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa watendaji wa Kata kusimamia afua za lishe kwenye Kata wanazoziongoza. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji.
Akifafanua zaidi amesema lengo la Tanzania kufanikiwa kwenye uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 linahitaji kuwa na wananchi wenye afya bora itakayowezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi kwenye maeneo yao ya utendaji kazi.
Muwezeshaji wa mafunzo haya Afisa Lishe wa Jiji la Dodoma Semeni Juma aliwasisitiza Watendaji wa Kata kupanga, kutekeleza na kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa Halmashauri na afua za lishe. Lengo ikiwa ni kutokomeza ulishaji duni kwenye familia, maradhi ya mara kwa mara na kupiga vita huduma hafifu za malezi na makuzi ya awali kwa watoto wadogo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.