SERIKALI imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Mama na Mtoto Jijini Dodoma ili kuimarisha huduma za tiba kwa magonjwa ya wanawake na watoto.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/23 leo Jumatatu tarehe 16/05/2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Ummy alikuwa amefafanua juu ya utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa katika bajeti ya mwaka 2022/23. Amesema kuwa Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ukiwemo huo wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto.
Waziri Ummy amevitaja vipaumbele ilivyojiwekea Wizara ya Afya katika mwaka wa fedha 2022/23 ili kuboresha huduma za afya nchini ni kama vifuatavyo: -
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.