• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Watumishi wa Afya watakiwa kuhakikisha dawa za tiba zenye asili ya kulevya zinadhibitiwa

Imewekwa tarehe: May 11th, 2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

WATUMISHI wa afya katika Mkoa wa Dodoma wametakiwa kuhakikisha dawa za tiba zenye asili ya kulevya zinadhibitiwa ili kuondoa mianya ya dawa hizo kutumika tofauti ya lengo lililokusudiwa na kusababisha uraibu wa dawa za kulevya katika jamii.

Rai hiyo ilitolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Nelson Buruku wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa dawa za tiba zenye asili ya kulevya katika hospitali na vituo vya afya vinavyotumia dawa hizo mkoani Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Tawi la Dodoma.

Dkt. Buruku alisema “kwa kutambua kuwa ninyi watumishi wa afya ni watu wa awali mnaokutana na wagonjwa na kuwapa matibabu mna jukumu la kuhakikisha dawa za tiba zenye asili ya kulevya zinadhibitiwa ipasavyo ili kuondoa mianya ya matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo kwa jamii. Hivyo basi, ninawaomba kupitia mafunzo haya ambayo wengine ni kwa mara ya kwanza lakini wapo ambao walishawahi kupata mafunzo haya siku za nyuma kuhakikisha mnayaishi katika utendaji kazi wenu ili kuwezesha matumizi sahihi ya dawa hizi”.

Alisema kuwa dawa hizo zinatumika katika kutibu na kupunguza maumivi. “Hivyo, pamoja na faida hiyo, dawa hizo zisipodhibitiwa vizuri huweza kuleta madhara kwa jamii hasa zikitua katika mikono isiyo sahihi. Natoa rai kwenu watumishi mnaosimamia dawa hizi kuepuka vishawishi vitakavyosababisha uchepushwaji wa dawa hizi na kupelekea mzigo kwa nchi kutibu waraibu wa dawa za kulevya” alisema Dkt. Buruku.

Akiongelea matarajio yake kwa washiriki, alisema kuwa mafunzo hayo yatatoa uelewa wa pamoja. Alisema kuwa maazimio yatakayowekwa yatakuwa shirikishi na yatatekelezwa kwa ufanisi ili kulinda afya ya jamii na kulipunguzia taifa janga la matumizi yasiyo sahihi ya dawa za tiba zenye asili ya kulevya.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Kati, Benedict Brashi alisema kuwa mamlaka imetoa mafunzo kwa vituo vinavyotumia na kutunza za tiba zenye asili ya kulevya. “Mafunzo haya yanahusisha vituo 47, yakijumuisha maeneo ya namna vituo vinavyoweza kununua dawa, kutunza na kutumia. Dawa hizi zinaleta madhara na utegemezi. Mafunzo haya tunapitishana kwenye muongozo wa TMDA unaoshughulikia udhibiti wa dawa hizi ili dawa hizi zisitumike ndivyo sivyo na zinawafikia walengwa” alisema Brashi.

Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba Kanda ya Kati inahudumia mikoa minne ya Dodoma, Morogoro, Iringa na Singida ikiwa na jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba, vitendanishi, tumbaku na mazao yake.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.