MKURUGENZI wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Bi. Ziada Sellah amekemea matumizi ya simu kwa wauguzi na wakunga wakati wa kazi, amewataka watumie simu zao kutangaza shughuli za uuguzi na ukunga ili kukuza zaidi sifa ya kada hiyo.
Bi. Ziada alisema simu unaweza ukaitumia vizuri ama ukaitumia vibaya, akatole mfano kuwa kama wakati wa kazi utakuwa unasoma kwenye whatsapp kuona vioja gani vimetumwa, utakuwa unasikiliza, unasoma, kucheka, unafurahi, hata mgonjwa akiita kule huwezi kusikia. Tayari kunakuwa hakuna ule wajibu wa nesi ambaye ni muwajibikaji na mtu wa karibu kwa mgonjwa kuwa mbali na mteja wake.
Aliwakumbusha kuwa mgonjwa anapoita anatamani uitike haraka, lakini ukiwa busy kwenye simu huwezi kumsikia mgonjwa kama ameita! Matumizi ya namna hii ni matumizi yasiyofaa. Bi. Ziada akakazia kuwa simu inaweza kuwa chanzo cha maambukizi kama utakuwa unamhudumia mgonjwa, mara umeshika simu umeweka mfukoni, unamhudumia mgonjwa hujanawa unapokea tena simu, unakuwa unaeneza maambukizi wewe mwenyewe.
"Hebu tujitahidi sisi wenyewe kujikanya matumizi ya siku wakati wa kazi, wauguzi na wakunga wenzangu, kikubwa ni kuboresha huduma za kiuguzi na kiukunga ili tuweze kuhakikisha wateja wetu wanaridhika na huduma ambazo sisi tunawapa" alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi Ziada akakumbusha pia simu ikitumika ipasavyo inaweza kuwa ya faida kwa kutangaza huduma zao, akawasisitiza wauguzi na wakunga hao kuwa wao ndio ambao tunatakiwa kutoa faraja kwa wateja wao.
Chanzo: wizara_afyatz (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.