• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Wauguzi, Wakunga wasio na leseni kufutwa

Imewekwa tarehe: August 4th, 2020

Wauguzi na Wakunga ambao watakuwa hawajahuhisha leseni zao ndani ya miezi sita kuchukuliwa hatua, ikiwemo kufutwa kwenye daftari la Uuguzi na Ukunga, hivyo kutoruhusiwa kutoa huduma kwenye vituo vya afya vya umma au binafsi.

Hayo yamesmwa leo na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Bi. Agnes Mtawa kwenye kikao kazi cha kuwajengea uwezo  wa kusimamia maadili na utendaji kazi Wauguzi wakuu wa Wilaya kinachoendelea jijini Dodoma.

“Nitoe rai kwa Wauguzi na Wakunga ambao hawajahuisha leseni zao ndani ya miezi sita, sheria inamtaka msajili awafute katika daftari la Uuguzi na Ukunga, na kama watafutwa hawatakuwa na sifa ya uuguzi na ukunga”. Alisema Bi. Mtawa.

Aidha, Msajili huyo alisema hadi sasa ni asilimia 75 ya wauguzi na wakunga ambao wameshahuisha leseni zao na asilimia 25 waliobaki bado wanaendelea kuangalia kwenye kanzidata yao kwani wapo wauguzi ambao pengine wamefariki, kustaafu na wengine wamebadilisha kada ila kwa wale ambao bado wanatoa huduma za uuguzi na ukunga wanakumbushwa kuwa na leseni iliyo hai kwa mujibu wa sheria ya Uuguzi na Ukunga Namba moja ya mwaka 2010, na kwa wale watakaoshindwa kuhuisha leseni, sheria inasema kwamba hawaruhusiwi kuendelea kutoa huduma ya Uuguzi na Ukunga.

“Taarifa imeshapelekwa kwa wahusika  na orodha imetayarishwa  kwa wale waliohuisha na wale ambao hawajahuhisha  watakuwa wamejifuta wenyewe na hawatokuwa na sifa ya kuendelea kutoa huduma za afya na waajiri wao watatakiwa kuwachukulia hatua za kuwafuta kazi kwenye vituo vya umma na vile vya binafsi.

Hata hivyo Bi. Agnes Mtawa amewakumbusha Wauguzi kuzingatia maadili kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria  kwani  kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale kuhusu utoaji wa huduma kwenye vituo vya afya hivyo kuwakutanisha wauguzi wakuu wa Wilaya kama viongozi na wasimamizi ni chachu katika kukumbushana taratibu na jinsi ya kusimamia miongozo na kanuni.

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Kalidushi Charles alisema malalamiko mengi yanaelekezwa kwa wauguzi kwani sehemu kubwa wao ndio wanaokaa na wagonjwa kwa muda mrefu na ndio watu wa kwanza kupokea wagonjwa hivyo wanapaswa kusimamia sheria, huku akisisitiza kuwa wasioneane haya bali wawajibishane ili huduma za afya ziwe nzuri.

“Tunafahamu sasa hivi serikali ya awamu ya tano imeboresha miundombinu, kumekuwa na vituo vingi vya kutolea huduma za afya ambavyo vinafanya upasuaji kwahiyo vituo hivi havitokuwa na maana kama sisi wasimamizi wa hizo huduma hatutosimamia vizuri ili wananchi waweze kupata huduma kama azma yake Rais”.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Wakuu wa Wauguzi ambaye ni Muuguzi kiongozi  kutoka  Wilaya ya Bukombe Fadhiri Meshack amesema kuwa,  mafunzo hayo yanawajengea uwezo viongozi kwa ajili ya kupanua wigo wa uelewa ili kuweza kuwasimamia na kuwasaidia wauguzi wanaowaongoza.

Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Bi.Agness Mtawa akikazia jambo wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wa kusimamia maadili na utendaji wa wauguzi na wakunga kinachoendelea Jijini Dodoma.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Bwana Kalidushi Charlse akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga kinachoendelea Jijini Dodoma,

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.